KILA KITU KIZURI KINAHITAJI MIPAKA

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na mtoto mmoja aliyeitwa Amani. Amani alikuwa anapenda sana kucheza lakini hakupenda kusikiliza ushauri wa wazazi wake.

Siku moja alipokuwa akicheza nje ya nyumba alimwona mzee mmoja aliyekuwa na simu ya ajabu. Simu ile ilikuwa inang’aa kama nyota.

Mzee akamwambia “Mtoto wangu hii simu ina uwezo wa kutimiza unachotamani lakini lazima uitumie kwa busara.”

Amani akapewa simu ile. Alipoomba pipi zikajitokeza. Alipoomba toys zikaja nyingi. Amani akafurahi sana.

Lakini baada ya muda simu ikaanza kumchosha. Alipokuwa akicheza sana akasahau kula, kusoma na hata kulala. Akawa mchovu na mwenye huzuni.

Siku moja simu ikazima. Amani akaanza kulia ndipo mzee yule akatokea tena na kusema

“Kila kitu kizuri kinahitaji mipaka.”Amani akaelewa kosa lake. Akaamua kutumia muda wake vizuri: kusoma, kucheza kidogo, na kusaidia nyumbani. Tangu siku ile, Amani akawa mtoto mwenye nidhamu.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments