KIBURI HUMUACHA MTU PEKE YAKE

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikua na msichana mmoja anayeitwa Linda. Linda alikuwa mwerevu na anapendeza lakini alikuwa na kiburi kwa wazazi wake.

Mama akimwambia apange chumba Linda husema “Ah sina muda na vitu vidogo vidogo!”

Baba akimuomba amsalimie jirani yeye hujibu

“Hiyo si kazi yangu.”

Siku moja umeme ulikatika wakati mama yake yuko kazini na baba yake yuko safarini. Linda alikuwa peke yake nyumbani. Alikuwa amezoea wazazi wake kufanya kila kitu hivyo hakujua taa za dharura zilihifadhiwa wapi wala hakujua kuwasha jokofu la dharura lililotumia betri.

Muda ulienda giza likawa nene na simu yake ikazima chaji. Linda akaanza kuhisi hofu kwa sababu hakuwa na msaada.

Kweli jirani yule ambaye hakutaka kumsalimia alipita na kugundua Linda yu gizani. Akamletea tochi na msaada. Linda alihisi aibu kwani hakuwahi kuwa mkarimu kwa jirani huyo.

Mama yake aliporudi Linda alimkimbilia na kusema

“Samahani Mama… leo nimegundua kuwa bila nyinyi mambo mengi hayaendi. Nitaanza kusaidia.”Mama yake akamkumbatia na kusema

“Heshima na unyenyekevu humjenga mtoto.”

Tangu siku ile Linda alibadilika alikuwa msikivu, mnyenyekevu na mwenye kusaidia. Wazazi wake wakafurahi sana kuona mabadiliko yake.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments