KALAMU YA UKWELI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na mtoto wa kike aliyeitwa Neema. Neema aliishi na mama yake katika nyumba ndogo karibu na soko la kijiji. Mama yake alikuwa akiuza mboga ili kupata pesa za matumizi ya nyumbani.

Kila asubuhi Neema alikuwa akiamka mapema kumsaidia mama yake kuosha vyombo, kufagia nyumba na kupanga mboga. Baada ya kazi hizo Neema aliandaa begi lake na kwenda shule. Alipenda kusoma ingawa wakati mwingine alikuwa akichoka.

Siku moja shuleni rafiki yake alimpa kalamu nzuri mpya na kumwambia

“Nimeipata darasani.”

Lakini Neema alihisi kuwa kalamu ile huenda ilikuwa ya mtu mwingine. Alikumbuka jinsi mama yake alivyomfundisha kuwa kuchukua kisicho chako si jambo jema.

Wakati wa mapumziko Neema alimfuata mwalimu na kumkabidhi kalamu ile. Baadaye msichana mmoja alilia kwa furaha aliporudishiwa kalamu yake. Mwalimu alimpongeza Neema mbele ya darasa lote.



Jioni aliporudi nyumbani Neema alimweleza mama yake kilichotokea. Mama yake alitabasamu na kusema

“Uaminifu wako ni mali kubwa kuliko pesa.”

Neema alilala akiwa na furaha akijua amefanya jambo sahihi.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments