Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikua na mvulana mdogo aitwaye Tito. Tito alikuwa na miaka 9 na alipenda sana wanyama lakini familia yake ilikuwa maskini na hawakuweza kumununulia mnyama wa kufuga.
Siku moja Tito alipokuwa anarudi kutoka shuleni alisikia mbwa akilia karibu na jalala la kijiji. Alipokaribia alimkuta mbwa mdogo, mwembamba na mchafu akiwa amejeruhiwa kwenye mguu.
Tito alimwonea huruma. Akakaa chini na kumgusa mbwa yule
Aliamua kumbeba mbwa hadi nyumbani. Mama yake alipoona alishtuka kidogo lakini alipoona jeraha la mbwa yule akasema
“Ni vizuri kumsaidia. Lakini tutamuweka nje mpaka apone.”
Tito alimuita mbwa Simba kwa sababu ingawa alikuwa mdogo macho yake yalionesha ujasiri.
Kila siku baada ya shule Tito alikuwa anamwosha Simba kumsafisha jeraha na kumpa chakula walichokuwa nacho hata kama kilikuwa kidogo. Polepole Simba akaanza kupona. Alikuwa akimfuata Tito kila mahali kama rafiki wa kweli.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment