Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Mitandao ya kijamii imekuwa sehemu ya maisha ya watoto wengi katika dunia ya sasa. Mitandao hii ina athari chanya na hasi kulingana na jinsi watoto wanavyoitumia. Kwa upande chanya mitandao ya kijamii huwasaidia watoto kujifunza mambo mapya, kupata taarifa za kielimu na kuwasiliana na marafiki zao walioko mbali. Hali hii huchangia kukuza maarifa na ujuzi wa mawasiliano.
Hata hivyo matumizi yasiyo sahihi ya mitandao ya kijamii yanaweza kuleta madhara kwa watoto. Watoto wanaweza kupoteza muda wa masomo, kuiga tabia mbaya wanazoona mtandaoni na kukutana na maudhui yasiyofaa kwa umri wao. Pia unyanyasaji wa mtandaoni unaweza kuwaathiri kisaikolojia na kuwafanya wajihisi vibaya.
Kwa upande wa afya matumizi ya muda mrefu ya mitandao ya kijamii yanaweza kusababisha matatizo ya macho, usingizi duni na kukosa mazoezi ya mwili. Hivyo wazazi na walezi wanapaswa kusimamia matumizi ya mitandao ya kijamii na kuwafundisha watoto kuitumia kwa njia sahihi ili iwe na manufaa zaidi kuliko madhara.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment