Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na panya mdogo aliyeishi karibu na shamba. Alipenda sana kujenga shimo lake la siri ambalo lingemlinda kutoka kwa wanyama wakubwa na hatari za msituni. Kila siku panya mdogo alichukua kidogo kidogo akatupa udongo nje ya shimo, na kuendelea kuchimba polepole.
Wanyama wengine walimuona akichimba shimo na wakacheka. “Panya mdogo unatumia muda mwingi sana na hatutajua kama shimo lako litakuwa kubwa” walisema. Lakini panya mdogo hakusikia maneno yao alijua kuwa kwa uvumilivu na bidii anaweza kufanikisha lengo lake.
Siku moja mvua ilianza kunyesha sana. Wanyama wakubwa walijaribu kujihifadhi lakini hawakuwa na makazi salama. Shimo la panya mdogo lilikuwa salama kabisa na hakuathirika. Panya alifurahi sana na kujivunia kazi yake.
Wanyama walijifunza kuwa bidii, uvumilivu na kufanya mambo hatua kwa hatua hutoa matokeo mazuri. Pia inatufundisha kuwa si lazima tumsikilize kila mtu anayekosoa bali tuendelee kwa imani na ujasiri katika kufanikisha malengo yetu.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment