
Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na kuku mmoja aliyeitwa Mama Kuku. Aliishi karibu na shamba pamoja na vifaranga wake. Kila siku aliwaonya vifaranga wake “Muwe makini msitoke mbali kuna mwewe hatari.”
Lakini kifaranga mmoja aitwaye hakusikiliza. Siku moja alitoka mbali na wenzake akicheza peke yake. Ghafla mwewe alitokea angani akitaka kumchukua.
Mama Kuku aliona hatari hiyo na akaanza kupiga kelele kwa sauti kubwa. Kuku wengine wote wa shamba walijiunga kupiga kelele. Mwewe akaogopa na kukimbia.
Kifaranga akarudi kwa Mama Kuku akiwa anaogopa sana. Akasema “Samahani Mama sitorudia tena.”
Mama Kuku akamkumbatia na kusema “Kumsikiliza mzazi huokoa maisha.”
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment