FAIDA ZA TUNDA LA PAPAI KWA WATOTO

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Tunda la papai ni mojawapo ya matunda yenye virutubisho vingi vinavyoweza kusaidia sana afya ya watoto. Watoto wanapokuwa katika hatua ya kukua miili yao huhitaji vitamini na madini mbalimbali ili kujenga kinga ya mwili, mifupa imara na maendeleo mazuri ya ubongo. Papai ni tunda linalopatikana kwa urahisi na linaweza kuliwa na watoto wa rika tofauti jambo linalolifanya kuwa muhimu katika lishe ya kila siku.

Papai linasaidia sana katika mmeng’enyo wa chakula. Tunda hili lina nyuzinyuzi na kimeng’enyo maalum kinachoitwa papain ambacho husaidia kuvunjavunja chakula tumboni. Watoto wengi hupata matatizo kama kukosa choo au tumbo kujaa gesi lakini ulaji wa papai mara kwa mara unaweza kuwasaidia kuepuka matatizo hayo. Hivyo papai huchangia kufanya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula ufanye kazi vizuri.

Papai husaidia kuimarisha ngozi ya mtoto. Vitamini C zilizomo ndani yake husaidia kufanya ngozi kuwa laini na yenye afya. Watoto wanaopata upele mdogo mdogo au muwasho kwenye ngozi wanaweza kufaidika kwa kula papai mara kwa mara.

 Tunda la papai ni muhimu sana kwa afya ya watoto. Ni tunda tamu rahisi kulila na lenye virutubisho vingi vinavyoweza kumsaidia mtoto katika hatua zake za ukuaji. Wazazi wanashauriwa kuwapatia watoto wao papai mara kwa mara ili kuboresha afya zao na kuimarisha ustawi wao kwa ujumla.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872




0/Post a Comment/Comments