Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na mtoto mmoja mzuri aliyeitwa Ashura. Ashura alikuwa anaishi na mama yake. Alikuwa mtoto mtiifu lakini mara nyingi alikuwa anaogopa giza.
Kila jioni giza lilipoanza kuingia Ashura alikuwa akijificha ndani ya nyumba. “Mama naogopa giza" alisema kwa sauti ya huzuni.
Siku moja mama yake alimpa taa ndogo na kumwambia, “Ashura taa hii itakusaidia. Lakini kumbuka ujasiri unatoka moyoni.”
Usiku ule umeme ulikatika. Nyumba ikawa giza. Ashura akaogopa sana lakini akakumbuka maneno ya mama yake. Akawasha taa ile na kukaa kimya.
Akiwa na taa mkononi Ashura akaona paka mdogo nje aliyekuwa analia. Bila kuogopa akatoka nje na kumsaidia paka yule.
Tangu siku ile Ashura akagundua kuwa ujasiri hauji kwa kukosa hofu bali kwa kufanya lililo jema hata ukiwa unaogopa.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment