Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na msichana mdogo aitwaye Zuri. Aliishi na bibi yake karibu na msitu mdogo wenye ndege wa rangi za kuvutia. Siku moja Zuri alipokuwa akicheza nyuma ya nyumba aliona mlango mdogo wa mbao uliokuwa umefichika kwenye kichaka.
Alishangaa sana.
“Mbona sijawahi kuuona huu mlango?” aliuliza.
Kwa ujasiri Zuri alifungua mlango. Mara tu alipoingia ndani alijikuta kwenye dunia ya ajabu yenye maua yanayozungumza vipepeo vinavyong’aa kama taa na mto uliokuwa ukitoa sauti ya muziki.
Maua yakamkaribisha “Karibu Zuri! Tumekuwa tukikusubiri.”
Zuri akashangaa “Kwa nini?”
Kiongozi wa maua lililoitwa Dafina likasema “Dunia yetu inahitaji msaada tumepoteza rangi zetu na wewe ndiye uliye na nguvu ya kuturudishia.”
Zuri akasema “Nitafanyaje?” Dafina likamwonyesha kibuyu cha rangi ya dhahabu. “Mwaga tone moja tu kwenye kila ua kwenye njia hii.”
Zuri alianza kazi. Aliweka tone moja kwenye ua la kwanza mara rangi zikawaka na ua likacheza kama limefurahi. Akaendelea hadi mwisho wa njia. Dunia yote ikarudia kuwa na mwanga na rangi.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment