URAFIKI HUANZA NA WEMA MDOGO TU

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na sungura mdogo aitwaye Timo. Timo alipenda kukimbia na kucheza lakini alikuwa hana marafiki wengi kwa sababu alikuwa mwoga kuongea na wanyama wengine.

Siku moja alipokuwa akiruka ruka msituni aliona mti mkubwa wenye maandishi

"Anayetaka rafiki awe rafiki."

Timo alisimama na kufikiria. Akaamua kuanza kwa tabia ndogo. Akamwona kobe akibeba mzigo mzito. Timo akasema "Kobe naweza kukusaidia?"

Kobe akafurahi na akasema "Asante sana Timo!"

Walicheka pamoja na kuendelea safari.

Kesho yake Timo alimsaidia ndege aliyedondosha kiota chake na siku iliyofuata akacheza na paa ambaye hakuwa na wenzi.

Baada ya siku chache Timo akashangaa kuona wanyama wote wakimuita

"Timo! Njoo tucheze!"

Sasa alikuwa na marafiki wengi kuliko alivyowahi kufikiria.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments