UPENDO WA WAZAZI HUISHI DAIMA MIOYONI MWETU

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na mtoto mdogo aitwaye Shukuru. Alikuwa na wazazi waliompenda sana. Walimfundisha kuwa mtiifu mwenye bidii na moyo wa kusaidia wengine.

Lakini siku moja kulitokea ajali mbaya ya gari na wazazi wake wote wakafariki. Shukuru alibaki peke yake akiwa na huzuni kubwa sana.

Kwa muda mrefu alihisi kama dunia yote imemgeuka. Kila usiku alilia kimya kimya akiwakumbuka wazazi wake. Lakini kila alipokumbuka maneno ya mama yake moyo wake ulipata faraja

 “Shukuru kamwe usikate tamaa. Mungu atakulinda na kukusaidia.”

Baada ya muda Shukuru alienda kuishi na bibi yake ambaye alimpenda kama mtoto wake mwenyewe. Bibi alimtia moyo kila siku akimwambia


“Wazazi wako wangependa kukuona ukifanya mambo makubwa.”

Maneno hayo yakampa nguvu mpya. Shukuru akaanza kusoma kwa bidii na kila siku alisema kwa moyo wa matumaini,

 “Nitakuwa daktari ili niwasaidie watu wengine na kufanya wazazi wangu wajivunie mbinguni.”

Miaka ikapita na Shukuru akawa kijana mwenye hekima, upendo na bidii. Alijifunza kuwa ingawa alipoteza wazazi wake hakuipoteza imani na ndoto zake.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments