UKWELI ULIONIFANYA NIKOSE USINGIZI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na kijana mmoja aitwaye Tunu aliyekua katika kijiji kidogo karibu na mto Ruaha. Tunu aliishi na baba yake Mzee Msola alikuwa mkali kupita kiasi. Alikuwa mkali si kwa sababu hakumpenda mwanawe bali kwa sababu maisha yalimfundisha kuwa ukali ndio njia pekee ya kuishi.

Tangu mama yake Tunu alipoaga dunia maisha yalibadilika. Mzee Msola alianza kuwa mkimya mwenye mawazo mengi na mara nyingi alionekana mwenye hasira zisizo na sababu. Tunu hakuielewa hali hiyo. Kila siku alitamani baba yake amkumbatie amwambie “Hongera” au “Ninafuraha kuwa na wewe” lakini hakuwahi kuyasikia maneno hayo.

Miaka ilivyopitaTunu alikua. Alipofika umri wa miaka kumi na nane alianza kuelewa kwa nini baba yake alikuwa mkali. Mzee Msola alimwambia

“Mwanangu nilikupenda tangu siku ya kwanza ulipozaliwa. Ila nilikuwa naogopa… nilikuwa naogopa nikikulea kwa upole sana maisha yatakupiga. Nilipoteza kila kitu kizuri nilichowahi kuwa nacho nikahofia nisi kupoteze wewe pia.”

Maneno hayo yalimgusa Tunu moyoni. Kwa mara ya kwanza aliona machozi yakitiririka usoni mwa baba yake machozi aliyodhani baba yake hangeweza kuyatoa.

Tunu alijifunza kuwa wakati mwingine malezi ya baba huwa magumu si kwa ukosefu wa upendo bali kwa wingi wa hofu ya kupoteza.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments