Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Amina alikuwa msichana mtiifu na mwenye bidii. Kila siku alipenda kujifunza mambo mapya na kuwasaidia wenzake darasani.
Siku moja walimu waliwaambia wanafunzi wafanye kazi nyumbani walete kesho yake. Amina alijaribu kufanya kazi hiyo jioni lakini taa ya nyumbani iliharibika. Hakumaliza kazi yake lakini aliamua asiseme uongo.
Asubuhi ilipofika watoto wengi walipoambiwa watoe kazi zao baadhi walidanganya wakisema walileta lakini zimepotea. Amina alisimama na kusema kwa sauti tulivu “Samahani mwalimu sikumaliza kazi yangu kwa sababu taa yetu iliharibika jana usiku. Naomba unipe nafasi nifanye leo jioni.”
Mwalimu alimwangalia Amina kwa tabasamu. “Umefanya vizuri kusema ukweli,” alisema. “Ninakuruhusu ukamilishe leo.” Wanafunzi wengine walijifunza kutoka kwake kuwa kusema ukweli ni jambo la heshima.
Kuanzia siku hiyo kila mwanafunzi alijitahidi kuwa mkweli kama Amina.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
.jpeg)

Post a Comment