Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na Panya aliyekuwa akiishi kwenye shimo dogo karibu na msitu. Ingawa alikuwa mdogo alikuwa mjanja na mwenye moyo wa huruma.
Siku moja mwindaji aliweka mtego mkubwa msituni ili akamate wanyama. Kwa bahati mbaya Simba alinaswa kwenye mtego huo na alianza kulia kwa sauti.
“Tafadhali nisaidieni! Nimekwama!”
Wanyama wengi waliogopa kumkaribia Simba lakini Panya alisema moyoni
“Simba ni mkubwa lakini bado anahitaji msaada kama viumbe wengine.”
Kwa ujasiri Panya alikimbia hadi pale alipokuwa Simba. Akaanza kung’ata kamba za mtego kwa meno yake madogo. Baada ya muda kamba zikakatika na Simba akawa huru!
Simba alimwangalia Panya kwa mshangao na akasema
“Asante sana rafiki yangu
SIkuamini kama mdogo kama wewe angeweza kuniokoa. Kuanzia leo nitakulinda siku zote.”
Panya akatabasamu na kujibu “Ukarimu hauhitaji ukubwa unahitaji moyo.”
Kuanzia siku hiyo Panya na Simba wakawa marafiki wakubwa na wanyama wote walijifunza kuwa kila mmoja ana uwezo bila kujali udogo wake.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment