Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na kijiji kidogo waliishi kwa amani lakini siku moja jambo la ajabu likatokea. Mvua kubwa ilinyesha sana ikasababisha mto kufurika. Wakati maji yalipojaa mtoto mdogo aliyeitwa Tunda aliteleza na kuangukia ndani ya mto. Watu wote wa kijijini walipatwa na hofu kwani maji yalikuwa mengi na yenye kasi.
Wote walipiga kelele “Tunda anaenda na maji! Msaada! Msaada!”
Lakini hakuna aliyethubutu kuingia majini walihofia kufa maji.
Ndipo Neema msichana mdogo wa miaka kumi tu akaona hali ile. Alikuwa mdogo kwa umri lakini moyo wake ulikuwa mkubwa kama simba. Bila kufikiri mara mbili Neema alikimbia hadi mtoni akachukua kamba iliyokuwa karibu akajifunga kiunoni na kumwambia baba yake.
“Baba shikilia hii kamba vizuri! Nitamtoa Tunda majini!”Watu wote walishangaa wengine wakamwambia, “Neema, usiende! Ni hatari!”
Lakini Neema aliingia majini kwa ujasiri akapambana na mawimbi makubwa hadi akamfikia Tunda. Kwa nguvu zote akamshika mkono na kupiga kelele.
“Vuteni kamba! Vuteni sasa!” Watu wa kijiji wakavuta kamba kwa pamoja hadi wote wawili wakatolewa salama kutoka majini.
Kijiji kizima kilishangilia “Hongera Neema! Wewe ni shujaa wetu!”
Tangu siku hiyo kila mtu kijijini alijifunza kuwa ushauri moyo wa huruma na ujasiri ni muhimu zaidi kuliko nguvu za mwili.
emakulatemsafiri@gmail.com
065393872


Post a Comment