SUNGURA NA MTI WA TUNDA MOJA

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Palikuwa na Sungura mdogo ambaye alikuwa mcheshi sana lakini alikuwa na tabia moja mbaya alipenda kufanya mambo kwa haraka bila kufikiria.

Siku moja wakati anazunguka porini Sungura aliona mti wa ajabu. Mti huo ulikuwa na tunda moja tu lakini lilikuwa kubwa jeusi na lenye harufu nzuri sana.

Sungura akasema hili tunda ni langu! Nitachuma mara moja!”

Lakini ndege aliyekuwa juu ya mti akamwambi “Sungura tunda hili linaweza kuanguka lenyewe likikomaa. Subiri tu kidogo.”

Sungura hakutaka kusubiri. Alijaribu kuruka juu alijaribu kukwea mti lakini mti ukawa mlaini na ukateleza. Alianguka mara tatu lakini bado alijaribu tena.

Sungura akajifunza somo kubwa si kila kitu kinahitaji haraka wakati mwingine ni bora kusubiri.

Tangu siku hiyo akawa Sungura mwenye subira na mwenye busara.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments