SIRI YA CHEMBE ZA DHAHABU


Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Amina alimkuta ndege mdogo amenasa kwenye miiba msituni. Bila kuogopa, akamtoa kwa upole hadi akawa huru kabisa.

Ndege akamshukuru sana na kumpa chembe tatu za dhahabu kama zawadi ya wema wake.

Amina alipokwenda kupanda chembe zile nyuma ya nyumba zikamea haraka na kutoa

Mti wa matunda makubwa na matamu Maua yenye harufu nzuri sana Na mti wa kivuli kizuri kilichowafanya watu wa kijiji kupumzika hapo.

Watu wote walishangaa miujiza ile na kumpongeza Amina kwa moyo wake wa huruma.

Tangu siku hiyo kijiji kiliishi kwa amani na furaha maana kila mtu alikumbuka kuwa ukifanya wema wema utakufuata.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments