Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Siku moja Gasto alipata ujumbe kwenye simu yake kutoka kwa rafiki yake wa karibu Terry. Ujumbe huo haukumlenga yeye lakini ulikuwa umetumwa kimakosa.
Huo ujumbe ulisomeka hivi
“Usimwamini Gasto kwenye ule mradi. Nitahakikisha hapati nafasi lazima nimpite.”
Moyo wa Gasto ulisimama. Terry alikuwa mtu aliyemsaidia kupitia magumu mengi mtu aliyempa chakula na ushauri. Lakini sasa alikuwa akiangusha jina lake kisiri.
Gasto hakupiga kelele wala hakumtukana.Alitafakari nini cha kumfanya rafiki msaliti kama huyu lakini hakupata majibu zaidi ya kutikisa kichwa na machozi yakimtoka utadhani mtoto aliyechapwa fimbo.
Baada muda kidogo alichukua simu yake na kuandika ujumbe mfupi lakini ulikua na maana kubwa sana alimwambia hivi tu
“Nimeona ujumbe wako sijakuumiza lakini umeniumiza. Kuanzia leo najua mahali pa kukuweka nakutakia siku njema.”
Na hapo urafiki wao ukaisha kimya kimya na kila mmoja akaendelea na maisha yake.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872

Post a Comment