Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na msichana mdogo aliyeitwa Neema. Alikuwa anaishi na wazazi wake Neema alipendwa sana na wazazi wake kwa sababu alikuwa mcheshi na mwenye bidii.
Siku moja mama yake alimwambia “Neema usiende kucheza mbali leo. Nenda dukani kanunue nyanya kisha urudi.”
Neema alikubali kwa sauti tamu “Sawa mama!”
Lakini alipokuwa akienda dukani aliona watoto wenzake wakicheza mbali karibu na mto. Akaanza kufikiri “Nikicheza kidogo tu si vibaya.”
Akaacha kwenda dukani na kukimbia kuwafuata. Wote wakaanza kucheza kurusha mawe majini na kuimba. Gafla mawingu meusi yakaanza kukusanyika angani mvua kubwa ikaanza kunyesha. Neema akakumbuka maneno ya mama yake lakini ilikuwa amechelewa.
Neema akarudi nyumbani akiwa amejaa matope na nguo zikiwa zimelowana na mvua. Mama yake alimkumbatia na kusema kwa upole
“Mwanangu si kwamba sikutaki ucheze lakini wazazi husema kwa sababu wanajali usalama wa watoto wao.”
Neema akatambua kosa lake na akaomba msamaha. Tangu siku hiyo alikuwa msikivu kwa wazazi wake na hakuwahi kupuuza tena maagizo yao.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment