Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na paka mdogo aliyeitwa Kido. Kido aliishi na mama kwenye nyumba yenye maua mengi mazuri. Ingawa Kido alikuwa mdogo lakin alikuwa na ndoto kubwa alitaka kuwa mlinzi jasiri wa wanyama wote wa kijijini.
Siku moja Kido alisikia ndege wakilia juu ya mti. “Chui! Chui!” walipiga kelele.
Kido bila kufikiria sana alikimbia kwenda kuona. Lakini alipofika chini ya mti aliona kwamba hakukuwa na chui. Ilikuwa ni upepo tu uliokuwa ukitikisa matawi.
Ndege wakamcheka “Kido wewe ni mdogo sana huwezi kuwa mlinzi!”
Kido alihuzunika sana. Lakini mama yake akamwambia
“Ujasiri haupimwi kwa ukubwa wa mwili bali kwa ukubwa wa moyo.”
Kesho yake kifaranga kidogo alianguka kutoka kwenye kiota. Wanyama wote walikuwa mbali, lakini Kido aliukimbilia ule mti kwa nguvu zote. Alilitumia jicho lake la makini na mikono yake midogo kumzuia yule kifaranga asiingie kwenye mtaro.
Ndege wakashuka na kumshukuru sana. “Tulikuwa tumekosea, Kido. Wewe kweli ni mlinzi wetu mdogo!”
Toka hapo Kido akawa mwenye kujiamini akijua kuwa ndoto zake zinaweza kutimia ikiwa ataamini katika nguvu zake.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment