Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Afya ni muhimu kwa kila mtoto na Nusrat ni mfano mzuri wa msichana anayejali mwili wake. Kila siku Nusrat huamka mapema huoga na kula kifungua kinywa chenye afya kama uji, chai na mkate. Mama yake humkumbusha kuwa chakula cha asubuhi huwapa watoto nguvu za kusoma na kucheza.
Nusrat pia hupenda kula matunda kama embe na parachichi baada ya kutoka shule. Anajua kuwa matunda husaidia mwili kupata vitamini. Zaidi ya hapo kila wakati kabla ya kula huosha mikono ili kuepuka magonjwa yanayotokana na uchafu. Tabia hii imemfanya asiwe mgonjwa mara kwa mara kama wengine.
Jioni Nusrat hufanya mazoezi madogo kama kuruka kamba. Mazoezi humsaidia kuimarisha mwili na kumfanya alale vizuri usiku. Kabla ya kulala hupiga mswaki ili meno yake yabaki safi na imara.
Kwa kifupi maisha ya Nusrat yanaonesha kuwa kutunza afya si jambo gumu. Ni kufanya mambo madogo kama kula vizuri kuzingatia usafi na kufanya mazoezi. Hizi ndizo tabia zinazomfanya Nusrat kuwa msichana mwenye nguvu na furaha kila siku.
0653903872


Post a Comment