Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
kulikuwa na kijiji kidogo kilichoitwa Lulanda ambacho usiku wake ulikuwa wa kipekee kila mtu angeweza kuona nyota zikicheza angani kama taa ndogo zinazocheza dansi. Watoto walipenda kuhesabu nyota hizo kabla ya kulala.
Lakini siku moja nyota zote zilipotea! Anga likawa giza kabisa. Watu wa kijiji wakahofia kuwa wachawi wabaya wamezichukua.
Msichana mmoja jasiri aitwaye Tunu akaamua kwenda kuzitafuta. Alibeba taa ndogo ya mafuta kipande cha mkate na kamba ya shaba aliyopewa na bibi yake.
Alipofika kwenye msitu wa Giza Nene alisikia sauti ikisema:
“Tunu unatafuta nyota? Utaweza kuzipata ikiwa moyo wako utang’aa kuliko taa yako.”
Tunu hakuelewa lakini aliendelea mbele. Alikutana na mnyama wa ajabu mwenye manyoya ya fedha ni Simba wa Anga. Simba huyo alimwambia
“Nyota zimefichwa ndani ya Pango la Kilio kwa sababu watu wameacha kuwa wema.”
Tunu akaahidi kurejesha wema kwa kila mtu atakayekutana naye. Njiani akasaidia ndege aliyejeruhiwa,akamgawia mkate mtoto aliyepotea.
Alipofika kwenye pango nyota zilianza kung’aa ndani ya kamba ya shaba aliyokuwa nayo zikijibu wema wake!
Tunu alizirudisha nyota angani. Tangu siku hiyo kijiji cha Lulanda kilijifunza kuwa mwanga wa kweli hauji kutoka angani.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment