MFALME WA MSITU ALIYEBADILIKA

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na simba mmoja aliyeishi msituni. Simba huyu alikuwa mkali sana. Wanyama wote walimwogopa kwa sababu kila siku alikuwa akiwafukuza na kuwatisha. Alipita huku na kule akijivunia. “Mimi ndiye mfalme wa msitu! Hakuna anayeweza kunikemea!”

Siku moja wanyama walifanya mkutano msituni. Sungura, fisi, tembo na ndege wote walikubaliana kwamba tabia ya simba ilikuwa imezidi. Lakini hakuna aliyethubutu kumkemea kwa sababu walijua atawashambulia.

Baada ya muda msitu ukaanza kukosa amani. Wanyama walikimbia, ndege wakahama na hata mito ilionekana kimya. Simba alibaki peke yake. Akawa hana mtu wa kuzungumza naye wala wa kucheza naye.

Siku moja simba aliugua. Alijaribu kuwatafuta marafiki wake lakini hakuna aliyekuja kumsaidia. Alilia sana.

“Ah! Laiti ningekuwa mwema kwa wanyama wenzangu wangenisaidia leo.” Simba alijiseamea peke yake.

Baada ya siku kadhaa sungura mdogo alisikia simba analia. Akiwa na moyo wa huruma alikwenda kumtembelea. Alimpa maji na matunda akamwambia

“Simba umeona sasa umuhimu wa kuwa mwema? Hakuna anayeishi peke yake.”

Simba alisema “Nimejifunza kosa langu sitakuwa mkali tena nitaishi kwa amani na wanyama wote.”

Kuanzia siku hiyo simba akawa mfalme mwenye upendo. Wanyama wote wakarudi msituni na msitu ukawa na furaha kama zamani.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments