MAZINGIRA NI UHAI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Zuri alipenda kwenda msituni kila asubuhi. Siku moja alipokuwa akikata maua alisikia sauti ikisema. “Zuri usivunje matawi yangu na nitakupa zawadi.”

Zuri akaogopa lakini sauti hiyo ilikuwa laini na yenye upole. Akauliza “Wewe ni nani?”

Mti ukamjibu “Mimi ni Mti wa Maisha. Ninalinda msitu huu. Watu wengi wanakata miti bila kufikiria na msitu unalia. Lakini wewe una moyo mwema.”

Zuri akashangaa. Akaanza kuongea na mti kila siku akijifunza mambo mengi kuhusu mimea wanyama, na siri za dunia. Kila aliposaidia kutunza msitu, maua yalichanua zaidi ndege walirejea na mvua ikanyesha kwa wakati.

Lakini siku moja baadhi ya wakazi wa kijiji walitaka kukata mti huo kwa mbao. Zuri akakimbia na kuwaomba wasifanye hivyo hawakumsikiliza.

Mti ukasema kwa huzuni “Zuri usilie nitajitoa ili wanakijiji wajifunze.”

Walipokata mti ardhi ikaanza kukauka mvua ikakoma na matunda yakakosa kuiva. Watu wakaelewa kosa lao wakamkumbuka Zuri na maneno ya mti. Wote wakaamua kupanda miti mipya na kuitunza vizuri.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments