KUJITUMA HULETA MAFANIKIO

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikua na Nyani Mjanja kwenye mti mkubwa katikati ya msitu. Nyani alikuwa mpweke lakini hakuwahi kukata tamaa. Kila siku aliamka na kusema.

“Leo nitafanya kitu kipya!”

Siku moja akaamua kujifunza kupasua nazi peke yake. Alijaribu kuipiga kwenye jiwe… ikaruka juu. Akajaribu kuibana kwenye tawi… ikamponyoka. Lakini Nyani hakukata tamaa.

Akasema “Kila tatizo lina njia yake.” Akatulia akafikiria kidogo kisha akaketi juu ya jiwe kubwa. Akaichukua nazi taratibu na kuipigiza chini paaa!

Nazi ikapasuka vizuri kabisa! Nyani akacheka kwa furaha “Huu ndio ujanja kujaribu tena na tena mpaka ufaulu.”

Tangu siku hiyo Nyani Mjanja alijua kuwa hata akiwa peke yake anaweza kufanya mambo makubwa kwa kutumia subira, kufikiri na kujaribu tena.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments