JUMA NA BAISKELI YA BABA

 


Emakulata Msafiri

 Mwanakwetukids

Juma alikuwa mvulana mdogo wa miaka kumi na moja aliyependa sana baiskeli. Kila jioni baada ya shule alikuwa akiwatazama marafiki zake wakipita mtaani kwao wakiendesha baiskeli zao wakicheka kwa furaha.

Wakati huo Juma alikuwa anatembea akibeba mkoba wake mgongoni akitamani siku moja naye awe na baiskeli yake.

Siku moja akiwa nyumbani alimwambia baba yake

 “Baba natamani sana kuwa na baiskeli lakini najua pesa ni ngumu. Nitaanza kuweka akiba yangu mwenyewe.”

Baba yake alisema Huo ni moyo mzuri mwanangu. Kila kitu kizuri kinapatikana kwa subira na bidii.”

Kuanzia siku hiyo Juma alianza kuweka akiba kidogo kidogo. Alikuwa anamsaidia mama yake kusafisha nyumba, kubeba maji na wakati mwingine kumsaidia jirani kubeba mifuko ya sokoni. Kila alipolipwa shilingi chache alikuwa anaweka kwenye kopo dogo aliloficha chini ya kitanda.

Miezi ikapita. Marafiki zake waliendelea kucheza na baiskeli zao lakini Juma hakukata tamaa. Alijua siku yake itafika.

Baada ya miezi sita kopo lilijaa. Baba yake alipohesabu pesa alishangaa kuona kwamba Juma alikuwa amehifadhi karibu nusu ya bei ya baiskeli ndogo. Baba yake aliongeza kiasi kilichobaki na wakaenda wote sokoni kununua baiskeli.

Juma alishika usukani wa baiskeli yake mpya kwa furaha isiyoelezeka. Alijifunza kuendesha kwa makini na kila alipomaliza kuitumia aliifuta na kuiweka vizuri.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments