Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
John alikuwa mvulana wa miaka tisa aliyependa sana kwenda shule. Kila asubuhi aliamka mapema na kujitayarisha kwa furaha. Lakini siku moja mambo hayakwenda kama kawaida.
Alipoanza kuvaa viatu vyake aligundua kuwa kiatu kimoja hakipo! John aliingiwa na hofu. Alianza kutafuta kila mahali chini ya kitanda nyuma ya mlango, sebuleni, jikoni na hata nje ya nyumba lakini hakukiona. Mama yake akamwambia “Tulia kidogo John kumbuka mara ya mwisho ulikivaa kilikuwa wapi.”
John akakumbuka kuwa jana jioni alikuwa akicheza mpira na marafiki zake nyuma ya nyumba. Akakimbia hadi uwanjani lakini bado hakukiona.
Wakati akizunguka kutafuta, irani yao Bibi Rehema alimwita
“John! njoo hapa mwanangu.”
John alipokaribia Bibi Rehema akamwonesha kiatu chake kilichokuwa kimekwama karibu na ua la mboga. John akashukuru sana na kukimbia kurudi nyumbani lakini tayari alikuwa amechelewa shule.
Kuanzia siku hiyo John aliweka viatu vyake sehemu moja maalum kila usiku kabla ya kulala. Hakupoteza tena kiatu.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment