JIKUBALI JINSI ULIVYO


Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Siku moja Kinyonga alikuwa akitembea taratibu kando ya barabara usiku. Ghafla akaona taa kubwa ya gari ikimulika kwa nguvu. Kinyonga akastaajabu na kusema

“Aaah! Hii taa inang’aa sana. Laiti na mimi ningekuwa na mwanga kama huo ningekuwa maarufu msituni!”

Kesho yake Kinyonga akaanza kujisifu mbele ya marafiki zake akisema

 “Mimi pia nitang’aa kuliko wote. Nitabadilisha rangi hadi iwe kama taa!”

Akatumia siku nzima akijaribu kung’aa zaidi. Lakini kadri alivyojaribu ndivyo alivyochoka na kupoteza rangi yake nzuri ya kijani. Wanyama wakamwangalia kwa huruma.

Jioni mvua kubwa ikaanza kunyesha. Gari lililokuwa na taa likazimika kwa sababu ya maji. Kinyonga akajificha chini ya jani. Baada ya muda taa ikaharibika lakini Kinyonga akabaki salama na mwenye amani.


Kesho yake wanyama walimwambia “Taa ilizimika lakini wewe bado upo salama. Tazama ulichokuwa nacho kilikuwa bora kuliko ulichotaka kuiga.”

Kinyonga akatabasamu na kusema “Sasa nimejua si kila kinachong’aa ni bora. Ni vizuri kujikubali kama ulivyo.”

emakulatemsafiri@gmail.com

0653902872


0/Post a Comment/Comments