FURAHA YA CHURA KWENYE NDOTO

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na chura mdogo aliyeitwa Bobo. Bobo alikuwa tofauti na vyura wengine hakupenda kuruka kwenye matope alitaka kuvaa miwani na suti kama binadamu!

Kila asubuhi Bobo alisimama kwenye kijito na kusema kwa sauti kubwa:

“Mimi ni Chura wa Kitaaluma! Sitaki kurukaruka bila mpango!”

Vyura wenzake walicheka sana. “Hahaha! Bobo chura wa suti! Utavaa tai kwenye bwawa?”

Lakini Bobo hakujali. Usiku mmoja alilala na kuota ndoto ya ajabu. Ndoto yake ilikuwa na malkia wa viumbe wa maji aliyeitwa Mama Samaki. Mama Samaki alimwambia

 “Bobo kama unataka kuwa chura wa heshima jaribu kufundisha wenzako nidhamu!”

Kesho yake Bobo alijaribu kufanya mazoezi ya nidhamu ya chura

“Chura wote simama mstari! Kuruka mara tatu kwa mpangilio!”

Vyura wote walijaribu lakini walicheka mpaka wakaruka hovyo-hovyo! Mvua ilianza kunyesha. kila mtu akateleza Bobo naye akaanguka ndani ya bwawa kwa kishindo!

Wote wakacheka sana hata Bobo mwenyewe akaanza kucheka.

Akasema “Sawa labda suti yangu haifai kwenye matope lakini angalau sasa wote tumekuwa marafiki wa nidhamu!”


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments