Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kuwasiliza watoto ni jambo muhimu katika malezi ya familia. Wazazi wanapowasikiliza watoto wao hujenga uhusiano wa karibu na wenye upendo. Mtoto anayejua kuwa sauti yake inathaminiwa hupata ujasiri wa kuongea na kueleza hisia zake bila woga. Hii huongeza imani kati ya mzazi na mtoto na kuifanya familia kuwa na amani zaidi.
Aidha kusikiliza watoto husaidia kugundua changamoto zao mapema. Mara nyingi watoto hupitia matatizo ya shuleni au kijamii na wanapopewa nafasi ya kuzungumza wazazi wanaweza kuwasaidia kabla mambo hayajaharibika. Pia mtoto anayesikilizwa hujifunza maadili mazuri kama kuheshimu, kutulia na kujenga hoja kwa upole.
Kwa jumla wazazi wanapowasikiliza watoto wao wanawajenga kuwa watu wazima walio na ujasiri, uelewa na tabia njema. Kusikiliza ni kitendo kidogo lakini kina matokeo makubwa katika maisha ya mtoto na familia kwa ujumla.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment