Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Baraka alikuwa mtoto wa miaka saba katika kijiji cha Mkwawa. Ingawa alikuwa mdogo watu walimjua kwa tabia yake ya kupenda kufikiria kabla ya kufanya jambo.
Siku moja ndoo ya kisima ilifunguka kwenye kamba na kuzama ya ndani ya kisima na bila ndoo hakuna aliyekuwa na maji ya kutumia. Wazee walikusanyika wakijaribu kufikiri suluhisho lakini hakuna lililofanikiwa.
Baraka aliyekuwa pembeni akasema kwa utulivu “Tujaribu kutumia kamba na jiwe dogo. Tunaweza kulinasa tundu la mpini.”
Watu wakampa nafasi Akafunga jiwe kwenye kamba kama ndoano akalishusha ndani ya kisima kwa makini.
Baada ya muda mfupi jiwe lilikamata mpini wa ndoo.Wakavuta ndoo juu polepole hadi ikatoka. Watu wakapiga makofi kwa furaha.
Mzee mmoja akamwambia “Baraka wewe ni mdogo kwa umbo lakini akili zako ni kubwa wanakijiji wakaanza kumwamini Baraka katika mambo mengi.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872

Post a Comment