WAZEE NI HAZINA YA MAARIFA

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Katika kijiji kimoja kilichozungukwa na milima na misitu aliishi kijana mmoja aitwaye Juma. Juma alikuwa kijana mwenye akili sana lakini alipenda kujiona kuwa anajua kila kitu. Alipenda kuwadharau wazee na hakupenda kushauriwa.

Siku moja Juma alimsikia mzee mmoja wa kijiji Mzee Ngeleja akiongea na watoto chini ya mti wa mkuyu. Mzee huyo alikuwa anajulikana kwa hekima na busara zake. Juma akaamua kwenda kumjaribu ili aoneshe kuwa yeye ni mwerevu kuliko wazee.

 “Mzee Ngeleja mimi nina swali. Kuna ndege mdogo nimekamata yuko mikononi mwangu. Je! ni hai au amekufa?”

Mzee akamtazama Juma akatabasamu kisha akamwambia “Jibu liko mikononi mwako mwanangu. Ukipenda awe hai ataishi Ukipenda afeatakufa.”

Juma akabaki kimya. Alitambua kuwa mzee alikuwa na hekima kubwa kuliko ujanja wake. Akaona aibu akamwachia ndege wake aruke kisha akamwambia. “Mzee nimejifunza si kila kitu najua na si kila kitu ninapaswa kujaribu.”

Tangu siku hiyo Juma alianza kuwaheshimu wazee na kusikiliza ushauri wao. Akawa kijana mwenye busara na kijiji kizima kikampenda.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments