Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Hapo zamani za kale aliishi msichana mdogo aitwaye Neema katika kijiji cha Mlimani. Alikuwa mtoto mwenye bidii lakini alikuwa hana subira. Alitaka kila kitu kipatikane haraka.
Siku moja babu yake alimpa mbegu ndogo ya mti wa matunda na kumwambia.
“Neema panda hii mbegu kwenye bustani. Ukihudumia vizuri siku moja itatoa matunda matamu.”
Neema alipanda mbegu hiyo kwa furaha. Kila siku alikwenda kuangalia kama imemea lakini siku ya kwanza hakukuwa na kitu. Siku ya pili bado. Siku ya tatu bado haijamea. Akakasirika na kusema.
“Babu mbegu yako ni mbovu! Sitaki tena!”
Lakini babu akatabasamu na kusema. “Vitu vizuri haviji haraka mwanangu. Endelea kumwagilia maji na kuwa na subira.”
Neema akasikiliza ushauri huo. Kila siku aliendelea kumwagilia mbegu hiyo. Baada ya wiki kadhaa mmea mdogo ukaota. Neema alifurahi sana akaendelea kuutunza akapalilia akaweka mbolea na kulinda dhidi ya wanyama.
Miezi ikapita mmea ukawa mti mkubwa wenye majani mazuri. Hatimaye siku moja Neema aliona maua yakichanua na baada ya muda kidogo matunda mazuri yakaanza kuiva.
Akamkimbilia babu yake akisema kwa furaha. “Babu! Angalia! Mti umezaa matunda!”
Babu akamwambia kwa upole “Umeona sasa? Uvumilivu huleta matokeo mazuri.”
Neema akatabasamu akakaa chini ya mti huo na kula tunda tamu sana tunda la uvumilivu wake.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
.jpeg)

.jpeg)
Post a Comment