USIOGOPE KUJARIBU


Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na ndege mdogo aliyeitwa Kushiki. Kushiki alikuwa na ndoto kubwa ya kuruka juu angani kama tai. Kila siku alitazama wenzake wakiruka kwa furaha lakini yeye alikuwa na hofu.

Siku moja mama yake akamwambia.

Usiogope ukijifunza kidogo kidogo utaweza kuruka juu pia."

Kushiki akaanza mazoezi. Mara ya kwanza alianguka mara ya pili akagonga tawi lakini hakukata tamaa. Kila siku alijaribu tena.


Hatimaye siku moja upepo mwanana ukavuma Kushiki akapanua mabawa yake akapaa juu juu zaidi ya kawaida. Akaimba:l

"Ninaweza! Ninaweza! Ninaweza!"

Wanyama wote walimshangilia. Kushiki  alifurahi kwa sababu aligundua kuwa siri ya kufanikiwa ni kujaribu tena na tena bila kuogopa kushindwa.

 

 

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872

0/Post a Comment/Comments