USIOGOPE CHANGAMOTO

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na ndege mdogo aliyeishi juu ya mti.Kila siku aliruka angani akiimba kwa furaha.

Siku moja upepo mkali ukavuma na Ndege yule akaogopa sana. Akafikiri

“Aha siwezi kuruka leo upepo utanipiga na kuniangusha chini!”

Lakini ndege wakubwa walikuwa bado wanaruka. Mmoja wao akamwambia

“Usiogope mdogo wangu. Ukijifunza kutumia nguvu za upepo vizuri zitakusaidia kuruka mbali zaidi.”



Ndege mdogo akajaribu kwa uoga. Mwanzoni upepo ulimyumbisha lakini akaendelea kupiga mbawa zake kwa nguvu.

Kadri alivyokuwa akijaribu ndivyo alivyozidi kuwa imara. Hatimaye akaanza kuelea vizuri angani.

Akaona kuwa upepo ule ule aliouogopa sasa unamsaidia kuruka juu zaidi!

Tangu siku hiyo ndege mdogo hakuwahi tena kuogopa upepo.

 

 

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872

0/Post a Comment/Comments