Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Palikuwa na familia ya ndege watatu Mama Ndege, Kido Ndege na dada yake Mdogo Ndege. Waliishi kwenye pori lilokua na furaha na Amani Tele.
Kila asubuhi Mama Ndege alikuwa akiruka mbali kutafuta chakula kwa ajili ya watoto wake. Kido Ndege alikuwa mzembe kidogo hakupenda kuruka wala kujifunza kuruka vizuri.
Siku moja upepo mkali ulivuma. Kiota chao kikatikisika sana hadi kutishia kuanguka. Mama Ndege aliporudi aliwaambia watoto wake.
“Watoto wangu ni lazima tujifunze kuwa na umoja. mmoja wetu akishindwa Jambo tushikamane kumsaidia.
Kesho yake upepo ulirudi tena. Kido Ndege na Dada Ndege wakasaidiana kushikilia kiota kwa kutumia vijiti walivyokusanya. Mama Ndege akawasaidia juu na kwa pamoja wakakilinda kiota kisibomoke.Baada ya upepo kupita Mama Ndege alisema kwa furaha.
“Mnaona sasa? Upendo na ushirikiano ndani ya familia ni nguvu kuliko upepo wowote.”
Tangu siku hiyo Kido Ndege alibadilika. Akawa mchapakazi na mtiifu kama dada yake. Familia ya ndege hao ikaendelea kuishi kwa amani na upendo mkubwa.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
.jpeg)
_in_tree_crop.jpg)
Post a Comment