TAMAA MBAYA

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Siku moja kulikuwa na ukame mkubwa. Wanyama wote walihangaika kutafuta maji. Sungura mjanja alisikia kuwa kulikuwa na kisima kidogo cha maji kimefichwa porini. Akaamua kwenda kunywa mwenyewe bila kumwambia yeyote.

Lakini fisi mwenye tamaa akamuona akienda kwa siri. Akaamua kumfuata. Sungura alipofika kisimani akaanza kunywa maji kidogo kwa staha. Fisi akaja kwa kasi na kusema.

“Eeeh Sungura we acha ujanja. Sasa mimi ndiye ninywe kwanza maana mimi ni mkubwa kuliko wewe!”

Sungura akamwambia

“Lakini maji haya ni machache tukinywa kwa heshima tutatosha wote.”



Lakini fisi akakataa akajitupa haraka kisimani akitaka kunywa yote. Kwa pupa yake akaanguka ndani ya kisima. Akajikuta amekwama na hawezi kutoka.

Sungura akacheka kidogo lakini akasema kwa hekima:

“Ndiyo maana nasema tamaa huleta hasara. Ukiridhika kila mmoja hupata.”

Wanyama wengine walipokuja waliona hali ya fisi na wote wakajifunza kuwa tamaa ni mbaya.

 

 

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872

 

 

 

 

 

 

 

 

0/Post a Comment/Comments