Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Siku moja shule yao iliandaa shindano la uandishi wa insha. Kila mwanafunzi alipaswa kuandika kuhusu mada “Ndoto Zangu za Baadaye”.
Emma alifurahi sana kwa sababu ndoto yake ni kuwa mwandishi wa habari. Alikuwa na kalamu moja tu ambayo aliipenda sana. Aliambiwa kwamba kalamu hiyo ndiyo ingemkumbusha ndoto yake kila anapoandika.
Siku ya shindano wakiwa darasani kalamu ya Emma ilianguka na kupasuka. Emma alishtuka na moyo wake ukaumia. Aliketi kimya huku machozi yakimlenga.
Wanafunzi wengine walicheka wakisema. “Hata kalamu imekataa ndoto zako!”
Lakini Allen alijisikia vibaya. Bila hata kufikiria mara mbili alimtoa kalamu yake mpya kabisa na kumpa Emma huku akisema:
“Ndoto zinaanza moyoni si kwenye kalamu. Chukua hii nimalize yangu baadaye.”
Emma alitazama kalamu hiyo na kisha akamkumbatia rafiki yake huku akisema
“Nitakumbuka siku hii maisha yangu yote. Rafiki kama wewe ni baraka.”
Emma akaandika insha yake kwa moyo wote na mwishoni wa shindano alishinda nafasi ya kwanza. Alipokuwa akipokea zawadi alisema mbele ya wote.
“Ushindi huu ni wetu mimi na Allen… kwa sababu mwandishi mzuri pia huhitaji rafiki mzuri.”
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment