Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na mvulana mdogo aitwaye Hassan mwanafunzi darasa la nne. Hassan alikuwa mtulivu na mwenye heshima. Siku moja mwalimu wao aliwaletea mtihani wa kushtukiza. Wanafunzi wote walitakiwa kufanya kimya bila kuangalia majibu ya wenzao. Hassan hakusoma vizuri alihofia kuanguka. Alimuangalia rafiki yake Amina na akaanza kunakili majibu yake kwa siri.
Baada ya mtihani mwalimu aligundua kuwa majibu ya Hassan na Amina yalikuwa yaleyale hadi makosa. Wote wakaambiwa wasimame darasani.
“Nani aliyeangalia majibu ya mwenzake?” mwalimu aliuliza.
Amina alilia na kusema, “Sikuandika kwa kuangalia kwa mtu nimeandika yale niliyokumbuka.”
Darasa lote liligeuka kumwangalia Hassan. Moyo wake ukaanza kumpiga kwa nguvu. Alijua amefanya kosa.Kwa hofu na aibu Hassan akainua mkono polepole na kusema kwa sauti ya chini.
“Ni mimi mwalimu... niliangalia majibu ya Amina. Samahani.” Darasa lilikaa kimya wengi walishangaa hawakutarajia Hassan aseme ukweli.
Mwalimu akamkaribia na kumwambia kwa upole.
“Kusema ukweli kunahitaji ujasiri. Leo naweka alama yako sifuri lakini umepata kitu kikubwa kuliko alama heshima na uaminifu.”
Amina akamsamehe Hassan na tangu siku hiyo.Hassan alijifunza kuwa ni heri uendelee kujifunza kuliko kudanganya.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment