PANYA ANYEPENDA MAHINDI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na panya mmoja mdogo aliyeishi kijijini. Alipenda sana mahindi kuliko chakula kingine chochote. Kila siku alikuwa akitoka pangoni kwake kwenda shambani kutafuta mahindi.

Kila alipofika shambani alikuwa anaiba mahindi na kuyabeba kidogo kidogo hadi nyumbani.

Wakulima wakaona mahindi yao yanapungua wakasema.

 “Lazima kuna mnyama anaiba haya mahindi. Tuweke mtego leo usiku.”

Usiku ulipofika panya akaenda tena shambani kama kawaida. Aliponusa harufu ya mahindi akaanza kutetemeka kwa furaha. Akasema.

 “Leo nitakula hadi nishibe!”

Lakini kabla hajajua akaingia kwenye mtego wa chuma uliokuwa umefichwa karibu na gunia la mahindi.

“Klaa!” mtego ukamkamata mkia wake!Panya akalia kwa maumivu “Aaah! Nimepatikana! Laiti ningesikia sauti ya moyo wangu kunikataza nisiondoke leo!”

Asubuhi yake mkulima alipomkuta alimwachia baada ya kumwonya

“Usirudi tena kuiba mahindi yangu.

Panya alirudi pangoni kwake akiwa ameumia na akaamua kuacha tamaa yake. Tangu siku hiyo alianza kulima sehemu ndogo nyuma ya pango lake akapanda mahindi yake mwenyewe.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments