Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Hapo zamani palikuwa na ndege mdogo aitwaye Chiriku. Chiriku alipenda kuimba kila asubuhi. Lakini hakukuwa na mti wa kukaa karibu na kijiji chake. Alihisi upweke sana.
Siku moja aliona mti mdogo ukikua pembezoni mwa shamba. Chiriku akasema.
“Mti mdogo, je! naweza kukaa juu ya matawi yako?”
Mti mdogo ukajibu,
“Ndiyo rafiki yangu ingawa mimi ni mdogo bado nitakushika.”
Tangu siku hiyo kila asubuhi Chiriku aliimba juu ya mti. Sauti yake iliwafurahisha watoto na wakulima wa kijiji. Kadri miaka ilivyopita mti ukakua mkubwa na Chiriku akawa na nyumba salama ya kuishi.
Mti na ndege wakawa marafiki wa kweli.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment