NDEGE ALIYEOGOPA KURUKA

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na ndege mdogo aliyeitwa Papi. Alikuwa na mabawa mazuri yenye manyoya meupe kama mawingu. Lakini tofauti na ndege wengine papi aliogopa kuruka juu angani.

Kila siku aliwaona wengine wakipaa kwa furaha wakipita juu ya miti na kujifurahisha angani. Walicheza na upepo walifanya mizunguko hewani na waliimba wimbo wa uhuru. Lakini Papi alikaa chini akisema.

“Nikiruka nitaanguka. Nikishindwa? Nikiumia?”

Siku moja upepo laini ulivuma ukagusa manyoya yake. Alihisi kitu moyoni hamu ndogo ya kujaribu. Akahema kidogo akapiga mabawa… FLAP! FLAP! …lakini akasimama tena.

Akasikia ndege wengine wakipita juu wakisema kwa sauti ya furaha.

“Hewa ni tamu! Anga ni pana! Usiogope kujaribu!”

Mwishowe Papi akachukua hatua ndogo. Akapiga mabawa tena… mara hii akainuka sentimita chache tu kutoka ardhini! Aliporudi chini moyo wake ukawa na furaha badala ya hofu.

Akasema kimoyomoyo.

“Kama niliweza kuinuka kidogo, basi naweza tena… na tena…”

Na siku iliyofuata aliruka juu kidogo zaidi. Kila jaribio likamfanya awe jasiri. Na hatimaye aliruka juu angani akacheka kwa furaha.

Hakukumbuka tena hofu alikumbuka tu hisia ya uhuru.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments