MLANGO USIO FUNGUKA ASUBUHI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kuna jengo refu mjini linaloitwa Kivuli Towers. Lina ghorofa nyingi lakini wakazi wote wa jengo hilo wanajua onyo moja.

 Usitumie lifti baada ya saa tatu usiku na usiwahi kwenda kwenye Ghorofa KIVULI.

Watoto wawili Neema na Jonas waliishi kwenye ghorofa ya tano. Walisikia tetesi kuwa Ghorofa Kivuli haipo mchana lakini usiku taa yake huwaka yenyewe kana kwamba kuna mtu anayeishi huko mtu asiyeonekana.

Usiku mmoja walichelewa kulala. Saa ilipofika 3:10 usiku lifti ililia “ting!” kama kawaida. Walidhani ni jirani anarudi lakini walipotazama koridoni hakukuwa na mtu hata mmoja.

Mlango wa lifti ulijifungua polepole. Ndani kulikuwa tupu lakini sauti ya kielektroniki ikasema kwa upole wa ajabu.

“Karibuni… Ghorofa KIVULI.” Wakiwa na udadisi wakaingia. Mlango ukajifunga wenyewe. Namba zilianza kupanda 6… 7… 8…

Badala ya kuonesha ghorofa inayofuata skrini ikazima na kupitia dirisha dogo waliona mji mwingine kimya kabisa hauna magari wala watu lakini vicheko vya watoto vilisikika kama vinatoka kwenye redio iliyoharibika.

Ghafla mlango mmoja mbele ukajifunga kwa kishindo kisha sauti nyembamba ya mtoto ikanong’ona ndani ya ukuta:

“Mlishaingia… Ghorofa KIVULI haiachii wageni.”

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903972


0/Post a Comment/Comments