Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na mbwa mmoja aliyeishi na kijana mdogo. Kila siku walicheza pamoja na kutembea shambani. Mbwa alimpenda sana kijana na kijana pia alimpenda mbwa wake.
Siku moja kijana alikwenda mtoni kuogelea. Alipokuwa ndani ya maji ghafla maji yakaanza kusonga kwa kasi na kijana akaanza kuzama. Alipiga kelele akiomba msaada lakini hakuna mtu aliyesikia.
Mbwa wake aliyekuwa ukingoni aliona rafiki yake akihangaika. Bila kusita mbwa akaruka majini. Kwa nguvu zake zote akamshika kijana kwa nguo na kumvuta kuelekea ufukweni. Hatimaye wakafika salama.
Kijana akamkumbatia mbwa wake akilia kwa furaha na kusema.
“Asante rafiki yangu wewe ndiye mlinzi wangu wa kweli.”
Tangu siku hiyo kijana alimlisha na kumtunza mbwa wake zaidi kuliko hapo awali. Na kila mtu kijijini alijua kwamba mbwa ni mnyama wa uaminifu na upendo mkubwa.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment