Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Siku moja kulikuwa na tembo mkubwa aliyeishi msituni pamoja na wanyama wengine wengi. Tembo huyu alikuwa mwenye nguvu lakini pia alikuwa mkarimu sana.
Siku moja ukame ulitokea. Mito ikakauka na wanyama wote wakaanza kuhangaika kutafuta maji. Wengine wakaanza kugombana na kupigana kila walipopata chemchemi ndogo.
Tembo akaamua kufanya jambo. Alichimba shimo kubwa kwa kutumia nguvu zake hadi maji yakaanza kutoka ardhini. Wanyama wote wakafurahia na wakaanza kunywa maji.
Lakini simba akasema “Tembo sisi wanyama wakubwa tutakunywa kwanza. Wale wadogo wangoje!”
Tembo akasema kwa sauti tulivu “Hapana maji haya ni kwa ajili ya wote. Hakuna mkubwa wala mdogo mbele ya kiu.
Wanyama wote wakasikia na wakakubaliana. Kuanzia siku hiyo waliheshimu tembo kwa hekima yake na upendo wake.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
%20(1).jpeg)

Post a Comment