KUTOKA KIBATARI HADI CHUO KIKUU

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na kijana mmoja aliyeitwa Samson aliyekuwa akiishi katika kijiji cha Tosamaganga Iringa. Maisha hayakuwa rahisi kwake. Baba yake alikuwa mkulima wa kawaida na mama yake aliuza mboga sokoni. Licha ya changamoto hizo Samson alikuwa na ndoto kubwa  alitaka kusoma hadi chuo kikuu na kubadilisha maisha ya familia yake.

Kila asubuhi Samson alitembea kilomita tano kwenda shuleni. Viatu vyake vilikuwa vimechakaa lakini moyo wake ulikuwa umejaa matumaini. Alipofika nyumbani alisaidia wazazi wake shambani kisha alikaa kusoma kwa mwanga wa kibatari. Wenzake walimcheka wakimwambia “Samson unasoma bure hakuna atakayekulipia shule ya sekondari!”



Lakini Samson hakukata tamaa.

Baada ya mitihani ya darasa la saba alipata alama za juu sana. Wazazi wake hawakuweza kumlipia ada laakini kutokana na bidii yake shule moja ya sekondari ya bweni ilimchukua kwa ufadhili wa masomo. Huko pia Samson aliendelea kufanya vizuri akawa kiongozi wa wanafunzi na mfano wa kuigwa.

Baada ya miaka kadhaa Samson alifanikiwa kufika chuo kikuu.Baada ya kuhitimu alirudi kijijini kwao akiwa na mpango wa kusaidia jamii. Kwa juhudi zake alianzisha mradi wa maji safi uliowasaidia mamia ya wakazi wa kijiji chake.

Wazazi wake walijaa furaha na vijana wengine wa kijiji walimwona Samson kama mfano wa kuigwa kijana ambaye hakuruhusu umasikini umzuie kufikia ndoto zake.

 

 

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872

0/Post a Comment/Comments