Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na Kipepeo mdogo aliyeishi ndani ya yai dogo kwenye tawi la mti. Kila siku alisikia sauti za ndege wakiimba na upepo ukipuliza majani lakini yeye alikuwa bado ndani ya yai akiogopa kutoka.
Siku moja Jua likamulika kwa upole juu yake na kusema kwa sauti ya upendo
“Kipepeo mdogo amka! Dunia inakusubiri usihofu kutoka nje.”
Lakini Kipepeo akasema kwa sauti ndogo “Sitaki kutoka nje kuna upepo, kuna mvua na kuna wanyama wakubwa. Nitabaki hapa.”
Jua likatabasamu na kusema “Kama hutatoka hutajua uzuri wa maisha. Wakati mwingine ujasiri mdogo unafungua milango mikubwa.”
Baada ya muda Kipepeo akachomoa kichwa chake taratibu kutoka kwenye ganda. Akaona mwanga mzuri wa asubuhi na maua yenye rangi akashangaa.
“Oooh! Dunia ni nzuri hivi?” Akaanza kupiga mabawa yake kwa hofu lakini Jua likamwambia
“Endelea usiogope! Mabawa yako ni imara kuliko unavyofikiri.”
Kipepeo akapaa juu kidogo kisha juu zaidi hadi akawa juu ya maua akicheza na upepo. Alijisikia huru mwenye furaha na jasiri.
Tangu siku hiyo kila asubuhi alipoona jua likichomoza Kipepeo alikuwa wa kwanza kupaa na kusema.
“Niliogopa lakini sasa najua ujasiri hufungua maisha mapya.”
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment