KIBURI SI MAUNGWANA

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na kijiji kinachoitwa Mapambazuko ambacho kilijulikana kwa amani na upendo. Kijijini hapo aliishi mvulana mmoja aitwaye Juma. Juma alikuwa mwenye akili nyingi shuleni na alipenda kujisifia sana. Kila alipofanya vizuri aliwaambia wenzake kwa sauti kubwa "Mimi ndiye bora kuliko nyote!"

Wenzake walihuzunika kwa sababu Juma hakuwa na unyenyekevu. Walimu wake mara nyingi walimkumbusha, "Kiburi hakijengi, Juma. Unyenyekevu ndio hufanya mtu akubalike." Lakini Juma hakusikia. Aliamini kuwa kwa sababu yeye ni mjanja basi ana haki ya kujiona zaidi ya wengine.

Siku moja kulikuwa na mashindano ya kijiji ya kukimbia. Watoto wote walijiandaa lakini Juma alisema "Hamna wa kunizidi. Nitashinda bila hata kujitahidi." Hakucheza mazoezi kama wenzake. Aliamua kukaa kivulini akijisifu.


Siku ya mashindano ilipofika watoto wote walikuwa tayari kwenye mstari. Walimu walipiga filimbi mashindano yakaanza. Wenzake waliokimbia kwa bidii wakapita mbele yake taratibu. Mwanzoni Juma alicheka na kusema "Bado nitawapita." Lakini muda ulivyosonga alichoka haraka kwa sababu hakuwa amefanya mazoezi.

Mwishoni Juma alifika mwisho kabisa. Wenzake walishangiliwa kwa sababu walijitahidi wakati Juma alikaa pembeni akiwa na aibu. Mwalimu alimsogelea kwa upole na kumwambia "Una akili Juma lakini bila unyenyekevu na bidii akili pekee haitoshi."

Juma akainama na kusema kwa sauti ya unyenyekevu "Nimejifunza. Kuanzia leo sitajisifu tena nitajitahidi na kuwaheshimu wenzangu."

Tangu siku hiyo Juma akawa mtoto mpole na mwenye bidii. Wenzake wakaanza kumpenda

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments