Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Siku moja kulikuwa na Sungura aliyeishi kwenye kichaka karibu na mto. Alikuwa mcheshi lakini pia mjanja sana. Kila siku alienda mtoni kuosha uso wake na kunywa maji safi.
Karibu na pale aliishi Fisi ambaye alikuwa mchoyo na mwenye tamaa. Fisi huyo kila mara alitaka kula wanyama wadogo bila kufanya kazi.
Siku moja Fisi alimwona Sungura akienda mtoni. Akasema kwa sauti ya chini “Leo nitampata huyu Sungura lazima nimle!”
Fisi alijificha nyuma ya kichaka akisubiri. Lakini Sungura alihisi harufu ya Fisi. Akacheka kimya kimya na kusema kwa sauti.
“Ah! Nimefurahi sana. Jana nilipata samaki mkubwa sana mtoni". Fisi alipolisikia hilo macho yake yakang’aa. Akafikiri.
“Samaki mkubwa? Huyu Sungura lazima aniwekee chakula!”
Sungura akaenda mtoni na kuanza kuchimba shimo dogo. Fisi akaenda haraka kumsaidia akidhani anachimba samaki. Lakini kumbevSungura alikuwa anachimba mtego!
Wakati Fisi amepinda kuangalia ndani ya shimo sungura akamsukuma kwa nguvu boooom! Fisi akaanguka ndani ya shimo.
Sungura akacheka na kusema “Tamaa mbaya huleta tabu! Kaa huko ujifunze!” Kisha akaondoka akirukaruka kwa furaha.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
.jpeg)

Post a Comment